CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU MKUU WA CHUO
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO
YAH: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KONGAMANO MAALUM LA VIONGOZI WA NGAZI
MBALIMBALI WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
KURUGENZI YA
KUDHIBITI NA KUSIMAMIA UBORA (DIRECTORATE OF QUALITY ASSURANCE AND CONTROL) YA
CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA ILIYO CHINI YA OFISI YA MAKAMU MKUU WA CHUO IMEANDAA
KONGAMANO LA SIKU MBILI KWA VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI KWA LENGO LA KUBORESHA
UTENDAJI WA KAZI WA KILA SIKU KATIKA MAENEO YAO NA HIVYO KUBORESHA HUDUMA NA
TIJA.
KONGAMANO HILO
LITAWASHIRIKISHA VIONGOZI WOTE WA JUU WA CHUO KUANZIA MAKAMU MKUU WA CHUO,
MANAIBU MAKAMU WAKUU WA CHUO ,WAKUU WA
VITIVO, WAKURUGENZI, WAKUU WA IDARA PAMOJA
NA WAKURUGENZI WOTE WA VITUO VYA MIKOA VYA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KUTOKA
TANZANIA BARA NA VISIWANI.
KATIKA
KONGAMANO HILO MADA MBALIMBALI ZINATARAJIWA KUWASILISHWA NA WATU MBALIMBALI
ZIKIWA ZIMELENGA KUIBUA NA KUONGEZA ARI YA UFANYAJI KAZI CHUONI NA HIVYO
KUZIDISHA KIWANGO CHA UFANISI WA UTOAJI WA HUDUMA BORA. MADA HIZO NI PAMOJA NA
MFUMO WA KI ELEKTONIA WA KUDHIBITI FEDHA, MUUNDO MPYA WA CHUO KIKUU HURIA CHA
TANZANIA, SERA NA MWENENDO WA UTENDAJI KAZINI, MASWALA YANAYOHUSU FEDHA KWA
VIONGOZI WASIOHUSIKA NA MAMBO YA FEDHA, MAWASILIANO THABITI NA MAHUSIANO BAINA
YA WATU, KAZI NA WAJIBU WA VIONGOZI WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA, MAJUKUMU NA
WAJIBU WA WAKUU WA VITIVO NA WAKURUGENZI, JINSI YA KUKABILI MABADILIKO KATIKA
TAASISI, MASWALA YAHUSUYO MAJALADA YA KIELEKTONIA (ELECTRONIC FILE MOVEMENT) NA
MASWALA YANAYOHUSU MANUNUZI YA UMMA.
MATARAJIO YA
KONGAMANO NI KUONGEZA WELEDI WA KIUTENDAJI NA TIJA PAMOJA NA KUBORESHA UTOAJI
WA HUDUMA KWA WATENDAJI WA NGAZI ZOTE CHUONI.
KONGAMANO HILO
LITAFANYIKA KATIKA HOTELI YA WHITE SANDS JIJINI DAR ES SALAAM SIKU ZA JUMAMOSI
TAREHE 09 MACHI, 2013 NA JUMAPILI TAREHE 10 MACHI, 2013 KUANZIA SAA MBILI
KAMILI ASUBUHI MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI.
KONGAMANO LITAFUNGULIWA RASMI NA
MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA PROF. TOLLY S.A. MBWETTE NA
KUFUNGWA NA NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO ANAYESHUGHULIKIA RASILIMALI PROF. MATERN
VICTOR.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU MKUU WA CHUO
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO
CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA- 07/03/2013
No comments:
Post a Comment